Wife Or Husband Quotes

Quotes tagged as "wife-or-husband" Showing 1-4 of 4
Enock Maregesi
“Kama umeamua kuoa au kuolewa ukiwa na umri wa kati ya miaka 18 na 40, kulingana na kanuni ya kuachana na ukapera (‘optimal stopping’) umri wa kuwa na msimamo kuhusiana na mtu utakayeoa au kuolewa naye ni baada tu ya kufikisha umri wa miaka 26. Kabla ya hapo kuna uwezekano ukakosa wachumba bora, baada ya hapo wachumba bora wanaweza kuanza kupotea, hivyo kukupunguzia uwezekano wa kumpata mke au mume aliye mwema.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Tovuti za miadi (‘dating sites’) hutumia ‘optimal stopping’ kuwachagulia watu wachumba wao. Wanachofanya ni kwamba wanachagua watu 100. Wanaondoa 37% ya kwanza ya wale ambao sifa zao haziendani na sifa unazozitaka. Kisha wanakuchagulia mtu waliyeona ni bora zaidi kuliko wote waliobakia. Huyo waliyekuchagulia anaweza kuwa mke au mume bora. Lakini Mungu ana mipango yake. Unaweza kushangaa mke au mume bora akatoka kwenye 37% ya wale walioachwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu anaweza kusema ana wachumba sita ambao anafikiria kuchagua mmoja kuwa mke au mume. Akichagua kiholela atakuwa na hakika 9% ya kumpata mwenza bora wa maisha. Lakini akitumia ‘optimal stopping’ atakuwa na hakika 37%!”
Enock Maregesi

“If you are not a gift for your wife, you may become a gift.”
Tamerlan Kuzgov